product.title

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Katika warsha hii tutatafuta kuelewa, kutambua, na kukiri wito wa kibinafsi wa Mungu, tukichunguza mienendo ya wito huo tunapoangalia karama, mamlaka na fursa anazotoa. Tutajadili masuala na maswali kuhusiana na kuishi wito wa Mungu na kuchunguza athari za kufanya huduma katika kanisa mjini. Kozi hii ni nyenzo muhimu sana kwa wale wanaozingatia wito wa Mungu katika maisha yao na ya wengine!

Mfululizo wa Kozi za Misingi ya Huduma ulitayarishwa kutokana na kozi teule zinazofundishwa katika seminari yetu, Hope School of Ministry. Mada na maarifa ya kozi hizi na zana hizi za kujifunzia ni ya msingi kwa huduma bora ya mijini, na bila shaka zitathibitika kuwa za thamani sana kwa yeyote anayetaka kuandaa viongozi katika makanisa ya mijini. Kozi zote za Misingi ya Huduma zimeundwa mahususi ili kuwasaidia viongozi kukua katika ujuzi wao wa Maandiko, theolojia, maisha ya Kikristo na huduma kwa vitendo.