product.title

Theolojia Katika Picha

Katika mkusanyo huu wa vielelezo na michoro, Dk. Davis anatoa mkusanyo wa picha uliojaa ufahamu ili kumsaidia mwanafunzi wa Bible na theolojia kuchunguza maana za dhana nyingi ngumu za Maandiko. Anasema katika Utangulizi, “Ingawa mchoro wakati mwingine unaweza kutolewa kama kibadala duni cha maelezo fasaha ya hoja kuhusu wazo au dhana, tamathali za semi, michoro, au alama nzuri, mara nyingi unaweza kuwa zana ya kutusaidia kupata ufahamu bora zaidi wa fumbo au siri fulani.. . . . Manabii na mitume mara nyingi walitumia taswira na mafumbo ili kuwasaidia watu wa Mungu kuelewa namna Mungu alivyolitazama jambo fulani au hali fulani, au kuelewa maana ya fumbo fulani au dhana ambayo Mungu alikuwa akiiwasilisha kwao.”

Mkusanyiko huu wa sasa una michoro kadhaa kuhusiana na mada mbalimbali za kibiblia na kitheolojia, yote ikiwa imebuniwa ili kukusaidia kufahamu vyema zaidi maana ya mafumbo ya Maandiko. Hiki ni chombo kinachofaa kwa wale wanaofundisha au kuhubiri, au wale wanafunzi wa Biblia wanaotamani kuona Neno la Mungu likifafanuliwa na kueleweka vyema kupitia picha, vielelezo, majedwali, na sitiari.