product.title

Module 3: Theolojia ya Kanisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu katika Yesu Kristo ni mojawapo ya mada zenye kuburudisha na muhimu zaidi katika Maandiko yote. Yesu wa Nazareti, kupitia kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake, ameinuliwa kuwa kichwa juu ya watu wake wapya, wale walioitwa kumwakilisha duniani na kutoa ushahidi wa Ufalme wake ambao tayari upo japo haujakamilika bado. Kuelewa jukumu la Kanisa katika mpango wa ufalme wa Mungu ni muhimu kwa kila eneo la maisha ya ufuasi wa kibinafsi na wa kusanyiko; hakuna ufuasi au wokovu mbali na tendo la Mungu la kuokoa kupitia Kanisa. Kufahamu kile ambacho Mungu anafanya ndani ya na kupitia watu wake kunampa kiongozi wa watu wa Mungu uwezo wa kumwakilisha kwa hekima na heshima. Kanisa limefunuliwa kwa namna ya kivuli katika kusudi kuu la Mungu la kujiletea utukufu kwa kuokoa jamii mpya ya wanadamu kupitia agano lake na Ibrahimu. Kupitia ibada, ushuhuda, na matendo mema, Kanisa katika vizazi vyote huonyesha sifa ya umoja, utakatifu, ukatoliki (yaani kwamba kanisa ni la ulimwengu mzima), na utume wa ushirika wake. Katika Kanisa, Mungu anaonyesha maisha ya ufalme wake na kutangaza fursa ya neema yake kwa ulimwengu.