product.title

Module 2: Ufalme wa Mungu

Kati ya mambo yote yaliyohubiriwa na kufundishwa na Yesu wa Nazareti, hakuna somo lolote lililo muhimu na lenye kubishaniwa kama habari ya Ufalme wa Mungu. Wasomi wote wa kihafidhina na wasomi huru wanakubali kwamba somo alilopenda zaidi Yesu, ambalo alihubiri na kufundisha mara nyingi zaidi, ni Ufalme wa Mungu. Lilikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango wake mkuu, na theolojia yake pendwa na ya moyo wote. Cha kusikitisha ni kwamba, Kanisa la kisasa linaonekana kutozingatia sana kile ambacho Yesu alikiona kuwa muhimu zaidi katika huduma yake ya kinabii na ya Kimasihi. Tumaini letu ni kwamba moyo wako utashikwa na hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha ya ufuasi wa kibinafsi na huduma.

Katika masomo manne, moduli hii inatoa taswira ya jumla ya Utawala wa Mungu, kwa kuanzia na mjadala wa jinsi ukuu na ubwana kamili wa Mungu ulivyopingwa na shetani na wenzi wa kwanza wa kibinadamu hadi kuanzishwa kwa utawala wa Mungu katika Yesu Kristo na kupata kwake mwili. Sasa kwa kuwa Bwana wetu Yesu amekufa, amefufuka, na kupaa mbinguni, Ufalme wa Mungu unatangazwa ulimwenguni kote na Kanisa lake. Utawala wa Mungu hivi karibuni utakamilika katika Ujio wa Pili wa Yesu, ambapo kifo, magonjwa, na maovu yote yatakomeshwa, mbingu na dunia zote zitafanywa upya, na Mungu atakuwa Yote katika Yote.