product.title

Module 14 - Mungu Roho Mtakatifu

Kuna kweli chache za kitheolojia katika historia ya Kanisa ambazo zimezua mabishano mengi, kutokubaliana, na mafarakano kama fundisho la Roho Mtakatifu. Kuanzia mabishano ya zamani kuhusu Utatu na fundisho la “procession” (yaani fundisho kuhusu nafsi ipi ya Utatu iliipeleka nafsi nyingine kutenda kazi) hadi kutokubaliana kwa siku za leo kuhusiana na ubatizo na karama za Roho Mtakatifu, kuna mengi ambayo yanaweza kutufanya tuliendee somo hili kwa tahadhari; lakini, ninatumai kwa dhati kwamba haitakuwa hivyo. Fundisho la Roho Mtakatifu ni kiini cha uelewa wetu kuhusu asili ya Mungu na namna tunavyoweza kuuishi uwepo wake hai katikati yetu.

Moduli hii inaangazia Nafsi na Kazi ya Roho Mtakatifu, ikianza na ushahidi wa kibiblia wa Mungu Roho Mtakatifu kama nafsi ya tatu ya Mungu mmoja aliye katika Utatu. Tunaanza somo letu kwa kuchunguza kile ambacho Biblia inaonyesha kuhusu Roho kama nafsi ya kiungu ambaye ni Mungu na anatenda kwa ufahamu kama Mungu. Pia tutazungumzia uhusiano wa Roho na Baba na Mwana, ambapo Yeye ni “Kifungo cha Upendo” kati yao na “Zawadi yao ya Upendo kwa Ulimwengu.” Kisha, tutaangazia asili ya ufunuo wa kinabii na kweli kwamba Roho ndiye anayevuvia na kuangazia Neno la Mungu, na kuwahakikisha wanadamu kwa habari ya dhambi, akituwezesha kushinda udanganyifu unaosababishwa na dhambi na kutuongoza kwenye toba ya kweli. Tunafunga somo letu kwa kuangalia kwa kina uwepo wenye nguvu wa Roho Mtakatifu, yaani, huduma yake ya neema na nguvu katika maisha ya wale wanaotubu na kuamini. Tutaelezea jukumu muhimu la Roho katika tendo kuzaliwa upya, kuasiliwa (kufanywa wana), ubatizo, karama, kukaa ndani mwamini, kutia muhuri, na utakaso. Hakika, Roho Mtakatifu analiwezesha Kanisa kutimiza utume wake ulimwenguni.